JC-RECORDS KAMPENI YA KUHAMASISHA JAMII JUU YA ULEMAVU WA NGOZI.
"Kama viungo vyetu watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) ndiyo vinaleta utajiri, basi sisi wenye ulemavu wa ngozi tungekua matajiri wakubwa zaidi." ~ Suleiman Magoma.
Suleiman Magoma ni rafiki wa karibu kwa jamii, muhamasishaji mwenye kiu yakuona jamii inabadili mtazamo wake juu suala zima la "Ualbino."
Yuko katika hatua za awali za safari yake kuelekea hatima ya ndoto zake yaani "Tanzania salama kwa watu wote wenye ulemavu wa ngozi."
Studio ya Jc-records na ndugu Suleiman Magoma tunaota ndoto moja hivyo kwa pamoja tunandaa nyenzo sauti kwa minajili ya kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya suala zima la ulemavu wa ngozi "Ualbino" na pia kwa pamoja kufanya kampeni ya kuishinikiza jamii kubeba jukumu la usalama wa watu wote wenye ulemavu wa ngozi.
#Ni jukumu letu sote#