KAZI ZINAZOFANYIKA JC-RECORDS.

5
JC-RECORDS ni studio ya kurekodi na kutengeneza mziki, pamoja na shughuli mbalimbali za kitaalamu za nyenzo sauti. Kazi zetu zinabeba ubora kwa kuzingatia mrejesho wa ufanisi katika kila kazi tunaiyoifanya. Tumejikita katika kufanya kazi nzuri na kuweka kiwango kipya katika shughuli zote, hususani kuandaa na kurekodi kazi zote za kitaalamu za mziki na zinazohusu nyenzo sauti. Tuna mpangilio rafiki wa kazi pamoja na mazingira mazuri ya kufanyia kazi, yanayonatoa nafasi ya utulivu na starehevu pia. Iwe ni msanii chipukizi au mwenye uzoefu katika shughuli za mziki, JC-RECORDS tunatoa huduma ya kuaandaa na kurekodi kazi zote kwa umakini stahiki. Kama unaweza kufikiri ni namna gani kazi yako ungependa ifanyike, ndivyo itakavyokuwa na kwa ufanisi zaidi chini ya JC-RECORDS. Tunafahamu kuwa kila mteja huwa na matakwa yake, tuko tayari kutoa msaada unaohitajika na kuifanikisha kazi katika muda muhususi. Tunatoa huduma zetu kwa malipo ya kiwango kidogo kinachoweza kufikiwa na mteja ndani ya bajeti yake, na kufanya kazi yake kwa ufanisi wa hali ya juu. Fedha ni jambo la tatu baada ya kipaji/mahitaji yako na ubinadamu wetu. JC-RECORDS ni chachu ya msingi wa sanaa iliyojizatiti katika kukuza na kuibua ubunifu katika kiwango cha juu. Tunanyambuka katika swala la muda wa ufanyaji kazi, hivyo tunapatikana muda wote. Tunashauri wateja kuwa na wazo la kiubunifu kabla ya kuanza kazi, tunaamini katika maono na hisia za mteja. JC-RECORDS imejengwa katika msingi wa kikanuni wa kuhakikisha mteja anatathmini na kukagua kazi iliyofanyika katika kila hatua kuanzia kuandaa,kurekodi na kuhitimisha. Hii hutoa fulsa kwa mteja kuipa uhai kazi yake katika hali ya asili ya upekee, na kufanikisha chagizo la hisia mguso kwa wapokeaji wa mwisho wa kazi yake. Kazi iliyoandaliwa kwa makini na kurekodiwa kwa ubora hutoa fulsa ya kuinua mapato, na ni nyenzo muhimu katika utambulisho wa kuinyanyua kazi husika. JC-RECORDS tuko hapa kufanikisha hilo, tuko hapa kuifanya kazi hiyo. JC-RECORDS Inafanya kazi zifuatazo: >>Kurekodi sauti za santuri (gramafoni). >>Kuandaa ala za aina zote za mziki. >>Kuandaa mchanganyiko wa ala na sauti. >>Kuandaa ala za filamu. >>Kuandaa matangazo ya redio. >>Kurekodi matangazo ya redio. >>Kurekodi demo (rekodi ambayo haijafanyiwa usanifu). >>Kusanifu rekodi ya ala na sauti. >>Uandaaji na kurekodi vitabu sauti. >>Uandishi wa vitabu sauti. >>Uandaaji wa ala za kipee za harusi, sherehe za kumbukumbu,na mengineyo. >>Tunaanda kazi za mashairi ya sauti ya kidini, kimapenzi, harusi, sherehe mbalimbali na kadhalika. >>Tunaanda hotuba za aina tofauti. >>Tunaanda na kurekodi mafunzo ya sauti ya kidini, kijamii, kisiasa, kimapenzi na mengineyo. >>Uandaaji na kurekodi tenzi za kumbukumbu. JC-RECORDS “Fedha ni Jambo La Tatu Baada Ya Kipaji/Mahitaji Yako na Ubinadamu Wetu” Tupigie simu: 0712/0713 266865, 0789 333646 na 0784 670 341. Tuko Tabata, Njia ya Kinyerezi, Mkabala na Bragaza Village Ltd/Mid Way Secondary.

5 comments: