Msanii Kutoka JC-RECORDS ASHINDA Nafasi ya FIESTA SUPER NYOTA.

0
Msanii wa lebo wa JC-RECORDS MULLAH Jr. amefanikiwa kupata nafasi ya uwakilishi wa mkoa wa Dar-es-salaam katika shindano la Fiesta Super Nyota. Kwa niaba ya JC-RECORDS tunampa pongezi kwa kudhihirisha uwezo na kipaji alichonacho. Mullah Jr. yuko pia katika maandalizi ya album yake na bila shaka atakuwa mmoja wa wasanii watakaofanya show katika jukwaa la Fiesta Jumamosi hii. Pongezi hizi zinaenda sambamba na pongezi kwa studio zilizotolewa na wadau wa mziki waliokuwepo sunciro siku ya jumapili, ambao walifurahishwa na kutiwa moyo baada ya kusikia Studio na lebo ya JC-RECORDS ina takribani miezi mitatu tu toka ianze kufanya kazi rasmi. Tunatazamia mafanikio makubwa zaidi kwa wasanii walio chini ya lebo ya JC-RECORDS.

0 comments: