KICHOCHEO CHA TUNGO BORA.

1

Uandishi wa nyimbo/tungo zenye kuvuta hisia hauji kwa bahati.
Mara zote tungo nzuri hutegemea zaidi mguso wa tenzi toka moyoni mwa mwandishi.
Lakini ni kipi kinacho chochea usanifu wa tungo nzuri zenye kuteka hisia?
Mara zote watunzi bora wa nyimbo hutanabaisha kuwa mazingira tulivu ndio kichocheo kikubwa cha ufanikishaji wa tungo bora.
Ni muhimu sana kwa muandishi yoyote mbali na kuwa na maono, ubunifu na mguso katika tungo fulani, ni lazima awepo katika mazingira  tulivu ambayo hayawezi kumuondolea umakini au kumchepua katika wazo lake la msingi lilobeba maudhui ya tungo yake.
Wapo wale wanaoweza kutengeneza tungo papo kwa hapo bila kujali mazingira aliyopo, lakini uzoefu wa wanatungo bora unaonyesha kuwa nyimbo ambazo zinaishi nyakati zote mara zote si tungo za papo kwa hapo.

1 comment: