Sehemu ya Pili- KUJIFUNZA KUGHANI MITINDO HURU.

1

6. Ghani kuhusu mazingira yalikozunguka, hii ni njia nzuri zaidi ya kuonyesha kuwa wewe unafanya mtindo huru.
Inavutia kumsikia mtu akighani kuhusu vyote vinavyoonekana mahali ulipo wakati wa kughani.

7. Jumuisha lugha ya maumbo katika mistari unayoghani.
Lugha ya maumbo huongeza ubunifu na hutia nguvu katika mistari ya kughani.

8. Rejea matukio yaliyotokea karibuni.
Moja ya njia za kuongeza ubunifu katika kughani mtindo huru ni kujumuisha mistari inayorejea matukio muhimu ya karibuni yaliyotokea.
Kwa mfano unaweza ghani "mi sio zana za kilimo nikatae posho, mi ni mr politician kama wa nakaya nagombea kuongezwa posho"

Katika mfano huo juu utaona kuwa nimetumia lugha ya maumbo, yani Zana Za Kilimo nikimaanisha ZZK natumaini kifupi hiki kinaeleweka nimemgusia nani. Halafu Mr. Politician wa Nakaya anawakilisha wanasiasa wenye tamaa kama nyimbo yake ilivyokuwa inajieleza, mwisho nikarejea suala la posho ambalo ni tukio linalozungumzwa zaidi kwa sasa.

9. Anzia pale mwenzako alipoishia.
Ubora na umakini katika kughani mtindo huru, huonekana dhahiri pale unapoweza kuendeleza ama kujibu mwenzako alichokighani bila kuanzisha ghani za jambo tofauti, hivyo ili kufanya vizuri mtindo huru ni lazima kujifunza kusikiliza kwa makini na kufikiri kichwani muendelezo wa ghani kama nilivyoelezea katika andiko lililopita.

10. Kujifunza kwa kusikiliza vilinge vya mitindo huru.
Unapopata muda wa kusikiliza watu wakighani katika vilinge vya mitindo huru unajifunza namna ya kucheza na maneno, matukio, mazingira na hata mionekano ya wahusika mbalimbali.
Pia inakupa fursa ya kutanua wigo wa kamusi yako kichwani ya misemo na nahau za mtaani.

1 comment: