NJIA RAHISI YA KUJIFUNZA KUGHANI KWA MITINDO HURU.

2

Ni rahisi kujifunza jinsi ya kufanya mtindo huru katika kughani.
Mitindo huru ni aina ya kughani inayotumika katika
vilinge au ukiwa peke yako, aina hii ya kughani hubebwa na mashairi ya papo kwa hapo.

Kuna njia kuu 10 za kujifunza kughani mitindo huru.
Leo tutazungumzia aina 5.

1. Anza taratibu, hakuna haja ya kughani kwa vina au kwa mpangilio wakati unaanza kujifunza mitindo huru. Tumia maneno rahisi yanayokujia kichwani.

2. Endelea kughani bila kusita, wakati wa kughani utafanya makosa, utashindwa kuoanisha maneno na hata kughani maneno yasiyo na mantiki. Lakini usisimame kughani.

3. Kubuni maneno ya kuziba mapungufu katika kughani, huu ni mwendelezo wa njia niliyoielezea hapo juu, pindi unaposhindwa kuoanisha maneno, au kukosea utamkaji, au kusita katika kughani basi unatakiwa kuwa na maneno rahisi ambayo unaweza kuyatumia kama viunganishi au mchepuko wa kuendeleza mtindo huru.

4. Ghani katika akili kabla ya mstari kuisha, hii ni njia ambayo wasanii bora katika mitindo huru huitumia, hii hukuwezesha kuwa na mwendelezo mzuri katika mtindo huru.

5. Andika vina, unapoandika ghani zako mbali mbali hukuwezesha kuwa na mistari au vina vichache ambavyo unaweza kuvitumia pindi unapofanya mtindo huru.
Katika mtindo huru hutakiwi kughani mashairi uliyoyaandika lakini kuna baadhi ya vina au mstari unaweza kuujumuisha ukioanisha na maneno uliyobuni toka kichwani papo kwa hapo.
Kuandika mashairi mara kwa mara kunakuwezesha kupata wigo mpana wa vina, mistari mifupi yenye ujazo wa kuteka hisia, kuchekesha ama tambo za kimashairi.

2 comments: